×

We use cookies to help make LingQ better. By visiting the site, you agree to our cookie policy.

image

Habari za UN, Watumishi wa umma wanachangia ujenzi wa mustakbali bora kwa wote: Guterres | | Habari za UN

Watumishi wa umma wanachangia ujenzi wa mustakbali bora kwa wote: Guterres | | Habari za UN

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya watumishi wa umma, ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mchango wao ni muhimu sana katika ufanikishaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuhakikisha mustakbali bora kwa wote.

Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema lengo lake ni kuwaenzi wanawake na wanaume kote duniani ambao huwajibika kwa jukumu muhimu zaidi la kutoa huduma kwa umaa.

Amesema maadhimisho ya siku ya mwaka huu yanakuja wakati Dunia iko katikati ya kuelekea ukomo wa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu na hivyo amesisitiza kuwa “ Watumishi wa umma na taasisi wanazoziunga mkono zitakuwa muhimu zaidi huku ulimwengu ukiharakisha hatua za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo yako yanakwenda kombo.”

Ameichagiza dunia kwamba ili kutimiza malengo hayo “ Teknolojia lazima iwe kiini cha kuongeza kasi hii ya utekelezaji. Kila siku, teknolojia mpya zinaibuka ambazo zinashikilia uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyoishi na kufanya kazi. Inapotumiwa na utumishi wa umma wenye ujuzi, uliowezeshwa na wenye vifaa, teknolojia inaweza kuboresha ufikiaji na ufanisi wa huduma za umma, huku ikisukuma maendeleo kuelekea utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.”

Amehitimisha ujumbe wake kwa wito kwamba “Wakati tukiadimisha siku hii muhimu hebu tusherehekee sio tu kazi ya utumishi wa umma kote duniani lakini tutafute njia mpya za kutumia ubunifu katika kazi zetu na kuenzi uwajibikaji wa watumishi hao wa kufanyakazi kwa ushirikiano ili kujenga mustakbali bora kwa watu wote.”

Watumishi wa umma wanachangia ujenzi wa mustakbali bora kwa wote: Guterres | | Habari za UN Beamte tragen zum Aufbau einer besseren Zukunft für alle bei: Guterres | UN-Nachrichten Public servants contribute to building a better future for all: Guterres | UN news Les fonctionnaires contribuent à construire un avenir meilleur pour tous, affirme António Guterres | Actualités de l'ONU Servidores públicos contribuem para construir um futuro melhor para todos: Guterres | notícias da ONU Offentliga tjänstemän bidrar till att bygga en bättre framtid för alla: Guterres | FN-nyheter

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya watumishi wa umma, ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mchango wao ni muhimu sana katika ufanikishaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuhakikisha mustakbali bora kwa wote.

Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema lengo lake ni kuwaenzi wanawake na wanaume kote duniani ambao huwajibika kwa jukumu muhimu zaidi la kutoa huduma kwa umaa. |||message|||||||||||||||||||||||||

Amesema maadhimisho ya siku ya mwaka huu yanakuja wakati Dunia iko katikati ya kuelekea ukomo wa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu na hivyo amesisitiza kuwa “ Watumishi wa umma na taasisi wanazoziunga mkono zitakuwa muhimu zaidi huku ulimwengu ukiharakisha hatua za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo yako yanakwenda kombo.” |commemoration||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||

Ameichagiza dunia kwamba ili kutimiza malengo hayo “ Teknolojia lazima iwe kiini cha kuongeza kasi hii ya utekelezaji. Kila siku, teknolojia mpya zinaibuka ambazo zinashikilia uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyoishi na kufanya kazi. Inapotumiwa na utumishi wa umma wenye ujuzi, uliowezeshwa na wenye vifaa, teknolojia inaweza kuboresha ufikiaji na ufanisi wa huduma za umma, huku ikisukuma maendeleo kuelekea utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.”

Amehitimisha ujumbe wake kwa wito kwamba “Wakati tukiadimisha siku hii muhimu hebu tusherehekee sio tu kazi ya utumishi wa umma kote duniani lakini tutafute njia mpya za kutumia ubunifu katika kazi zetu na kuenzi uwajibikaji wa watumishi hao wa kufanyakazi kwa ushirikiano ili kujenga mustakbali bora kwa watu wote.” ||||call|||commemorate|||||let's celebrate|||||||||||||||||||||||||||work|||||||||